IQNA

Duru ya mwisho ya mashindano ya hifdhi ya Qr'ani Oman

12:01 - April 12, 2011
Habari ID: 2104578
Duru ya mwisho ya mashindano ya 21 ya hifdhi na tajwidi ya Qur'ani Tukufu yaliyopewa jina la Sultan Qabus itafanyika mjini Muscat Oman hapo tarehe 23 Aprili.
Akizungumzia suala hilo Muhammad bin Abdallah as-Swaqri, mkuu wa idara ya wakfu na masuala ya kidini ya Oman amesema uwa mashindano hayo yatawashirikisha washindani kutoka pembe zote za nchi hiyo inayoongozwa kifalme. Amesema washindani wanaume na wanawake 42 walishiriki katika hatua ya kwanza ya mashindano hayo ambayo ilifanyika hapo siku ya Jumatatu. Amesema kuwa mashindano hayo ya kila mwaka yatakuwa yakifanyika katika miji mbalimbali ya nchi hiyo. 773002
captcha