. Kwa mujibu wa tovuti ya Zawya kikao hicho kimefanyika kwa lengo la kuoanisha masuala ya kifedha ya Kiislamu na hali halisi ya mambo katika soko la Mashariki ya Kati. Akizungumza katika kikao hicho, Muin ad-Deen Malim, Mkurugenzi Mwandamizi wa Shirika la Mashriq al-Islami ambalo limedhamini kikao hicho amesema kuwa uwekezaji wa Kiislamu ni muhimu sana katika eneo la Mashsriki ya Kati kwa kutilia maanani mahitaji mapya ya watumiaji wa bidhaa na huduma za benki za Kiislamu katika eneo. Huku akiashiria mashindano makali yaliyopo kati ya benki za Kiislamu na zisizo za Kiislamu katika kuwavutia wateja, Malim amesisitiza kuwa benki za Kiislamu zinapasa kuboresha huduma kwa wateja wao. Kikao hicho ambacho kimehudhuriwa na wataalamu mashuhuri wa masuala ya kifedha na uwekezaji imekuwa fursa nzuri kwa wawekezaji na wafanyakazi wa benki za Kiislamu kuchunguza fursa na changamoto zinazokabili shughuli zao. 773309