Ahmad Tayyib Sheikh wa al-Azhar amemtaka Papa Benedict wa XVI auombe rasmi msamaha ulimwengu wa Kiislamu kutokana na kukosewa heshima Qur'ani na matukufu mengine ya Kiislamu katika nchi za Magharibi na kusema kuwa hilo ni sharti muhimu la kuanzishwa tena mazungumzo ya kidini kati ya Uislamu na Ukristo.
Kwa mujibu wa gazeti la al-Ahram la nchini Misri, Sheikh Ahmad Tayyib ambaye alikutana na kuzungumza na Michael Gerald, balozi wa Vatican mjini Cairo hapo siku ya Jumanne amesema kuwa, uhusiano wa Waislamu na Wakristo wa Kanisa Katoliki hauna matatizo yoyote lakini kwamba uhusiano rasmi wa Waislamu na Papa Benedict ni baridi na kwamba al-Azhar inataraji kuwa kiongozi huyo wa Vatica atachukua hatua ya dharura ya kuwaomba rasmi msamaha Waislamu kuhusiana na dharau inayofanywa dhidi ya matukufu ya Kiislamu katika nchi za Magharibi. Amepinga kuanzishwa tena kwa mazungumzo ya kidini kati ya Uislamu na Ukristo kabla ya kuombwa rasmi Waislamu msamaha kuhusu jambo hilo.
Katika upande mwingine, kikao cha kwanza cha Beitul al-Aila kilifanyika jana Jumatano huko Cairo kwa uvumbuzi wa Sheikh Tayyib kwa lengo la kukabiliana na fitina za kidini nchini Misri. Viongozi na wawakilishi mbalimbali wa Kikristo na Kiislamu walihudhuria kikao hicho. 773963