IQNA

Rais Ahmadinejad: Uhusiano wa Iran na Lebanon umepindua njama za maadui wa nchi hizi

12:54 - April 17, 2011
Habari ID: 2107053
Rais Mahmoud Ahmadinejad wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa uhusiano mzuri na thabiti kati ya nchi yake na Lebanon umekuwa ukiwatia kiwewe maadui ambao lengo lao ni kuvuruga murua katika eneo la Mashariki ya Kati.
Akizungumza kwa njia ya simu na Spika wa Bunge la Lebanon Nabih Beri, Rais Ahmadinejad amesema kuwa njama za maadui dhidi ya Iran na Lebanon zimefeli kutokana na nchi mbili hizi kushirikiana kwa karibu na kuzungumza kwa sauti moja. Amesifia mitazamo sawa ya nchi hizo mbili katika masuala ya kieneo na kimataifa na kusema Lebanon imedhihirisha uadilifu wakati wote inapojadili masuala ya kieneo na kimataifa. Spika wa Bunge la Lebanon Nabih Beri kwa upande wake ameipongeza Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa kuwa kinara wa kutetea haki za walio wengi na vile vile kuwa kipaza sauti wa nchi zilizofinywa na kubanwa na Wamagharibi.
775339
captcha