IQNA

Larijani: Marekani taabani kwa kuanguka madikteta katika eneo la Mashariki ya Kati

13:01 - April 17, 2011
Habari ID: 2107060
Spika wa bunge la Iran amesema leo kuwa Marekani imejikuta taabani baada ya kuangushwa madikteta iliowalea kwa miongo kadhaa iliyopita katika eneo la Mashariki ya Kati.
Akizungumza wakati wa kufungua kikao cha bunge asubuhi ya leo, Ali Larijani amekosoa matamshi ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Hillary Clinton kwamba Iran inachochea machafuko katika eneo hili na kusisitiza kuwa Washington imejikuta katika hali ngumu na kwa mantiki hiyo inarusha maneno ovyo. Ali Larijani amesema kuwa Marekani imepoteza itibari katika eneo hili na kwamba kosa kubwa walilolifanya watawala wa Washington ni kudai kuwaunga mkono wananchi wanamapinduzi ilhali wamekuwa na uhusiano wa karibu na madikteta walioangushwa akiwemo Hosni Mubarak wa Misri na Zainul Abidin Bin Ali wa Tunisia.
775605

captcha