IQNA

Kiongozi wa Mashia wa Bahrain asisitiza udharura wa kufanyika marekebisho ya kisiasa

17:01 - April 17, 2011
Habari ID: 2107223
Akitoa radiamali yake kuhusiana na mauaji ya raia wa Bahrain wanaofanya maandamano ya amani kwa ajili ya kufanyika marekebisho ya kisiasa nchini humo, Ayatullah Isah Ahmad Kassim, kiongozi wa Mashia wa nchi hiyo amesisitiza juu ya udharura wa kufanyika marekebisho hayo na kwamba utawala wa nchi hiyo unapasa kutekeleza mpango madhubuti wa kufikiwa lengo hilo.
Akizungumza hivi karibuni katika swala ya Ijumaa katika msikiti wa Imam Swadiq (as) katika mji wa Durraz, Ayatullah Kassim amesema kwamba marekebisho hayapasi kusimamishwa katika jambo lolote lile isipokuwa lile lililoharamishwa na Mwenyezi Mungu. Amesema kila mtu anayekubali jukumu la uongozi na utawala anapasa kuwacha wazi mlango wa kufanyika marekebisho ili kupatikana uadilifu na usawa katika jamii. Sheikh Kassim amesisitiza kwamba Bahrain ni moja ya nchi zinazohitajia marekebisho makubwa ya kisiasa ili kufikiwa viwango vya demokrasia na kutekelezwa matakwa ya wananchi. Amesema serikali inayofaa ni ile inayotekeleza matakwa ya raia wake na kuongozwa na watawala wanaofaa. 775072
captcha