IQNA

Jamhuri ya Kiislamu ya Iran yatoa wito wa kuitishwa kikao cha dharura cha OIC

15:04 - April 18, 2011
Habari ID: 2107827
Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imetoa wito wa kuitishwa kikao cha dharura cha Jumuiya ya Nchi za Kiislamu OIC ili kujadili matukio yanayojiri hivi sasa katika Mashariki ya Kati na Kaskazini mwa Afrika.
Wito huo umetolewa na Dakta Ali Akbar Salehi, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ambaye amesisitiza kwamba, kuna haja kwa OIC kuitisha kikao hicho ili kujadili matukio yanayojiri hivi sasa katika ulimwengu wa Kiarabu. Katika barua yake kwa Profesa Ikmaludin Ihsanoglu ambaye ni Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Nchi za Kiislamu OIC, Dakta Salehi amesema kuwa, Iran iko tayari kuwa mwenyeji wa kikao hicho. Inafaa kuashiria hapa kuwa, hivi sasa nchini Bahrain, Yemen na Libya kunashuhudiwa ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu na mashirika pamoja na watetezi wengi wa haki za binadamu wamekuwa wakisisitiza haja ya kuchukuliwa hatua za lazima za kuhitimisha ukandamizaji dhidi ya raia katika nchi hizo.
776118
captcha