IQNA

Ahmadinejad: Mashariki ya Kati mpya itaibuka bila satwa ya Marekani na Utawala wa Kizayuni

17:12 - April 18, 2011
Habari ID: 2107901
Rais Mahmoud Ahmadinejad wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kwa yakini Mashariki ya Kati mpya itajitokeza pasina kuwepo tena satwa ya Marekani na Utawala wa Kizayuni na kwamba maadui wa mataifa hawana budi ila kukubali kushindwa na kusalimu amri mbele ya heshima ya mataifa.
Rais Mahmoud Ahmadinejad amesema kuwa, jeshi la Iran ndilo jeshi la wananchi zaidi, lenye nguvu zaidi na lenye izza kabisa miongoni mwa majeshi yote duniani. Akihutubu kando ya Haram ya Imam Khomeini kwa mnasaba wa Siku ya Jeshi hapa nchini, Dakta Ahmadinejad amesema bayana kwamba, jeshi ambalo linafanya harakati katika njia ya Mwenyezi Mungu katu haliwezi kushindwa. Rais Ahmadinejad amesema, taifa la Iran linapaswa kumshukuru Mwenyezi Mungu kwani katika kipindi chote hiki cha miaka 32, jeshi la Iran limeweza kuwa kifua mbele na kuzishinda njama zote za maadui wa taifa hili. Amebainisha kwamba, sababui ya jeshi la Iran kuwa na nguvu na uwezo mkubwa ni kushikamana na imani ya dini ya Kiislamu, kutegemea nguvu za ndani za wananchi na kujiamini huku likifanya hima na juhudi zisizokoma. Inafaa kuashiria hapa kuwa, leo ni Siku ya Jeshi hapa nchini Iran, sherehe ambazo kitaifa zinafanyika katika uwanja wa haram ya Imam Khomeini MA.
776120

captcha