Kwa mujibu wa tovuti ya Al Alam, Abdulrauf as-Shaib Msemaji wa muungano wa 'Februari 14' ametoa wito kwa ulimwengu wa Kiislamu ulaani jinai ya utawala wa Bahrain unapata himaya ya Marekani na Saudi Arabia. Ameongeza kuwa vikosi vya Ale Khalifa na Ale Saud vimevunjia heshima matukufu ya Kiislamu na kuchoma moto Qurani Tukufu sawa na alivyofanya kasisi mwenye misimamo mikali Terry Jones katika jimbo la Florida Marekani.
Kiongozi huyo wa upinzani ametoa wito kwa Umoja wa Mataifa uchukue hatua ya kuvilazimisha vikosi vamizi vya Saudia viondoke Bahrain. Aidha ametaka ummah wa Kiislamu uchukue hatua dhidi ya Ale Saud na Ale Khalifa.
777912