Dr. Hussein Ruyvaran, mtaalamu wa masuala ya Mashariki ya Kati amemwambia mwandishi wa IQNA kuwa mwamko wa Bahrain unawajumuisha watu waliowengi katika jamii ya nchi hiyo. 'Hii ndio sababu serikali ya Bahrain imefeli kukabiliana na mwamko huo na ikalazimika kuomba msaada wa kijeshi kutoka Saudia na Emarati kwa lengo la kuvunja maandamano".
Amesema uingiliaji wa nchi hizo mbili unakiuka sheria za kimataifa. Amesema kwa mujibu wa sheria za kimataifa, kila mtu ana haki ya kujiamulia mustakabali wake. Ameendelea kusema kuwa: "Saudia inajaribu kuhakikisha kuwa matukio ya Bahrain hayatavuka mpaka na kuingia nchini humo. Lakini kinyuma na hilo hali imeendelea kuwa mbaya Saudia baada ya watawala wa Riyadh kuingilia mambo ya ndani ya Bahrain.
Ameendelea kusema kuwa hivi sasa tunaona kuwa hata Masuni wa Saudi Arabia wanaipinga serikali katika hali ambayo huko zamani wapinzani walidaiwa kuwa tu katika mji wa Qatif". Hili linaonyesha wazi kuwa malengo ya watawala wa Saudia ya kuingilia kijeshi Bahrain yamefeli".
779350