Kwa mujibu wa tovuti ya Islamtoday, idara hiyo imedai kuwa sauti hizo zinaudhi na kuwasumbua walowezi wa Kiyahudi wanaoishi katika vitongoji vilivyojengwa kinyume cha sheria katika mji huo.
Akizungumzia suala hilo, Sheikh Muhammad Hussein, Mufti wa Quds Tukufu amesema kuwa takwa hilo la utawala haramu wa Israel ni katika juhudi za utawala huo za kutaka kuuyahudisha mji huo mtakatifu ili hatimaye wadai kuwa mji huo sio wa Kiislamu.
Maimamu wa misikiti na shakhsia wa Kiislamu wanaoishi katika mji huo pia wamesisitiza kuwa misikiti na minara ilijengwa katika mji huo hata kabla ya kubuniwa vitongoji vya walowezi wa Kiyahudi na kwamba walowezi hao wanapasa kuondoka mara moja katika mji huo. K
wa mujibu wa ripoti hiyo, awali Wazayuni waliwasilisha takwa hilo kwa meya wa Quds wakitaka kupigwa marufuku sauti zote za adhana kwenye misikiti ya mji huo. 782306