IQNA

Hukumu ya kifo kwa wapinzani, kukamilisha jinai za Aal Khalifa

16:47 - April 30, 2011
Habari ID: 2114573
Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Lebanon Hizbullah imetoa taarifa ikitangaza kuwa kutolewa hukumu ya kifo kwa wapinzani wanne wa malalamiko yanayoendelea dhidi ya ufalme wa Bahrain kunakamilisha jinai za ufalme wa ukoo wa Aal Khalifa dhidi ya Waislamu wa nchi hiyo.
Hizbullah imetangaza wasiwasi wake mkubwa kuhusiana na ukandamizaji pamoja na jinai zinazoendelea kufanywa na utawala huo dhidi ya waandamanaji wanaofanya maandamano ya amani dhidi ya ufalme huo kibaraka wa nchi za Magharibi.
Huku ikilaani hukumu ya kifo iliyotolewa dhidi ya waandamanaji wanne wa Bahrain, Hizbullah imesema kuwa hukumu hiyo ni ya kisiasa moja kwa moja na kwamba inakwenda kinyume na misingi ya sheria za nchi hiyo. Imesema kadiri utawala wa kifalme wa nchi hiyo utakavyojaribu kuonyesha kuwa hukumu hiyo ni ya kisheria lakini ni wazi kuwa hautafanikiwa kufunika sura mbaya ya ukandamizaji na jinai zinazofanywa na utawala huo dhidi ya raia wasio na hatia wa nchi hiyo wanaopigania kwa njia za amani haki zao za kimsingi.
Raia wanne hao wa Bahrain wamehukumiwa kifo kwa tuhuma zisizo na msingi eti za kuwaua askari polisi katika ghasia zinazoendelea kufanyika nchini humo. 782975
captcha