IQNA

Waislamu Azerbaijan wabanwa na wafuasi wa dini nyinginezo kupewa uhuru wa kuabudu

14:12 - May 01, 2011
Habari ID: 2115139
Katika hali ambayo serikali ya Azerbaijan imekuwa ikiwabana Waislamu wa nchi hiyo na kuwazuia kutekeleza majukumu yao ya kidini, serikali hiyohiyo imekuwa ikiwapa wafuasi wa dini nyinginezo fursa na uhuru kamili wa kutekeleza ibada na majukumu yao ya kidini.
Serikali ya Baku imekuwa ikitiliana saini na viongozi wa dini zisizo za Kiislamu mikataba ya kuwapa wafuasi wa dini hizo fursa na uhuru zaidi wa kutekeleza majukumu yao ya kidini bila kukabiliwa na vikwazo vyovyote vile kinyume na wanaovyofanyiwa Waislamu waliowengi wa nchi hiyo.
Waislamu wamekuwa wakifungiwa misikiti bila serikali kutoa sababu yoyote ya maana kuhusu jambo hilo.
Kwa mujibu wa mikataba iliyotiwa saini hivi karibuni kati ya viongozi wa Azerbaijan na Kanisa Katoliki, wafuasi wa kanisa hilo watakuwa na uhuru kamili wa kutekeleza majukumu yao ya kidini na kueneza shughuli zao nchini humo bila kukabiliwa na vikwazo vyovyote na hata ikilazimu, kupata msaada wa serikali katika kufikiwa lengo hilo. 784082
captcha