IQNA

Ulimwengu wa Kiislamu washuhudia zaidi ya majanga ya kibinadamu 90 mwaka 2010

15:21 - May 02, 2011
Habari ID: 2115844
Akizungumza katika kikao cha tatu cha wataalamu wa mashirika ya serikali yanayohusika na masuala ya kibinadamu huko Jeddah nchini Saudi Arabia, Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Nchi za Kiislamu OIC amesema kuwa ulimwengu wa Kiislamu mwaka uliopita wa 2010 ulishuhudia majanga ya kibinadamu 97 ambayo yalitokea katika nchi 32 za Kiislamu.
Amesema idadi hiyo inaunda asilimia 60 ya nchi zote wanachama wa OIC. Ekmeleddin Ihsanoglu Katibu Mkuu wa OIC amesema kwamba jamii ya kiraia ilikuwa na nafasi muhimu katika kudhibiti athari za majanga hayo na kutaka mashirika hayo ya kiraia yashirikishwe zaidi katika majanga kama hayo katika fremu ya shughuli za OIC. Amesema kufanywa hivyo kutaboresha utekelezaji wa majukumu ya OIC katika hali ya kutokea majanga ya kibinadamu katika pembe mbalimbali za ulimwengu wa Kiislamu. Kikao hicho cha Jeddah kilimalizika hapo jana Jumapili. 784245
captcha