IQNA

Rima Fakhri:

Jinai zinazofanyika Bahrain zinadhihirisha chuki ya utalawa wa Aal Khalifa kwa wananchi

17:53 - May 04, 2011
Habari ID: 2117535
Ukandamizaji mkubwa unaofanywa na utawala wa Aal Khalifa dhidi ya wananchi wa Bahrain na hukumu ya kifo liyotolewa dhidi ya wanaharakati wanne wa nchi hiyo vinaonyesha chuki kubwa ya utawala fisadi na wa kidikteta wa Aal Khalifa na Aal Saud dhidi ya wananchi wanaodhulumiwa wa Bahrain.
Hayo yamesema na Bi. Rima Fakhri, mwanachama wa Baraza la Kisiasa la harakati ya Hizbullah ya Lebanon katika mazungumzo yake na IQNA. Ameashiria vitendo vya kubakwa wanawake na kuvunjiwa heshima Qur'ani nchini Bahrain na akaongeza kuwa mambo hayo hayawezi kukubaliwa na yanalaaniwa na wanaharakati wote wa kutetea haki za binadamu.
Mwanafikra huyo wa Kiislamu amesisitiza kuwa ni wajibu kwa Waislamu wote kuwatetea watu wanaodhulumiwa na kukandamizwa na kuongeza kuwa uhalifu na jinai za kutisha zinazofanywa na utawala wa Aal Khalifa nchini Bahrain unagusa na kuumiza hisia za kila mtu huru hususan Waarabu na Waislamu.
Amesema Waislamu wote wanawajibika kushikamana na kuunda nguvu moja ya mashinikizo dhidi ya utawala fasidi na wa kidikteta wa Aal Khalifa huko Bahrain na vilevile jumuiya zinazoshirikiana na utawala huo dhidi ya wananchi ambao dhambi yao kubwa ni kudai haki zao za kisheria na kibinadamu. 786275

captcha