IQNA

Shirika la kupambana na ubaguzi ufaransa lakosoa marufuku dhidi ya akina mama wavaa-hijabu mashuleni

13:04 - May 05, 2011
Habari ID: 2117755
Taasisi Kuu ya Kupambana na Ubaguzi wa Rangi na Kutetea Usawa nchini Ufaransa HALDE imekosoa vikali marufuku inayotekelezwa dhidi ya akina mama wanaovaa hijabu katika baadhi ya shule za nchi hiyo.
Kwa mujibu wa tovuti ya atlasinfo taasisi hiyo imekosoa vikali uamuzi wa baadhi ya wasimamizi wa shule hizo wa kuwakosea heshima akina mama hao wa Kiislamu na kusema kuwa jambo hilo linakwenda kinyume na sheria za nchi hiyo.
Kwa mujibu wa sheria za Ufaransa akina mama wavaa-hijabu hawazuiwi kuandamana na watoto wao kwenye masomo ya ziada yaliyo nje ya ratiba za kawaida za masomo mashuleni, na ukiukaji wa jambo hilo unachukuliwa kuwa ni ishara ya wazi ya ubaguzi wa rangi.
Hivi karibuni baadhi ya shule za Ufaransa zimekuwa zikiwazuia wazazi wa wanafunzi Waislamu kuandamana nao katika ratiba za masomo zilizo nje ya ratiba za kawaida za masomo kwa kisingizio cha uvaaji hijabu. Hii ni katika hali ambayo ni wanafunzi wa kike tu ndio wanaozuiwa kuvaa hijabu wakati wa masomo na sio wazazi wao wa kike. Ni jambo hilo ndilo lililowafanya akina mama hao kuandamana siku ya Jumatatu wakilalamikia uonevu na dhulma hiyo inayofanywa dhidi yao na wakuu wa baadhi ya shule za nchi hiyo. 786695
captcha