IQNA

Makundi yanayopinga ubaguzi kufanya maandamano dhidi ya safari ya Geert Wilders nchini Canada

14:22 - May 10, 2011
Habari ID: 2119681
Makundi yanayopinga ubaguzi nchini Canada yanapanga kufanya maandamano makubwa kulalamikia safari ya Geert Wilders mbunge wa Uholanzi anayekosea heshima matukufu ya Kiislamu katika mji wa Toronto.
Kwa mujibu wa tovuti ya Canoe Wilders kiongozi wa chama chenye mielekeo ya kupindukia mipaka cha Uhuru na ambaye ametengeneza filamu ya dharau dhidi ya matukufu ya Kiislamu kwa jina la Fitna aliwasili mjini Toronto hapo siku ya Jumapili kwa lengo la eti kuwaonya Wacanada dhidi ya nchi yao kufanywa ya Kiislamu.
Akiwa mjini humo mbunge huyo anatazamiwa kutoa hotuba kadhaa kuhusiana na kile alichokitaja kuwa njia za kukabiliana na kuenea Uislamu duniani, lakini hadi sasa hakuna ratiba yoyote iliyotangazwa kuhusiana na sehemu atakazotolea hotuba hizo.
Vilevile imetangazwa kuwa watu watakaoruhusiwa kushiriki kwenye hotuba hizo ni wale tu watakaokuwa na barua za mwaliko.
Akiwa katika uwanja wa ndege wa Toronto, mbunge huyo mwovu ametoa matamshi ya kashfa na dharau dhidi ya Uislamu kwa kusema kuwa askari wa Canada hawakuuawa katika Vita vya Pili vya Dunia lakini wanakabiliwa na hatari ya kuuawa na kile alichokitaka kuwa eti idikteta wa fikra ya Uislamu.
Katika hali ambayo hakuna hata kundi wala jumuiya yoyote ya Kiislamu ambayo imetoa radiamali yake kuhusiana na kuwepo mbunge huyo wa Uholanzi nchini Canada lakini makundi ya kupinga ubaguzi yamesema kuwa yataandaa maandamano katika miji tofauti ya nchi hiyo kulalamikia suala hilo. 788897
captcha