Kongamano hilo linakusudia kuimarisha maelewano, hekima, na juhudi zenye kufuata uadilifu katika uga wa kimataifa katika kukabiliana na ugaidi.
Katika kongamano hilo kutakuwa na vikao vya kijadili maana ya ugaidi, misingi ya ugaidi, magaidi, uharibifu unaosababishwa na ugaidi na njia ya uadilifu ya kukabiliana na ugaidi.
Pembizoni mwa kikao hicho kutakuwa na maonyesho ya Wairani walioathiriwa na ugaidi.
Washiriki wa kongamano hilo la siku mbili pia watatembelea haram takatifu ya Imam Khomeini RA , muasisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
790906