IQNA

Wanawake Waislamu wa London kusherehekea uzawa wa Bibi Fatima Zahra (as)

12:20 - May 15, 2011
Habari ID: 2122351
Wanawake Waislamu wanaoishi mjini London Uingereza wanapanga kushiriki katika sherehe za kuadhimisha uzawa wa binti ya Mtume Mtukufu (saw) Bibi Fatima Zahra (as) ambazo zimepangwa kufanyika katika Kituo cha Kiislamu cha London hapo tarehe 24 Mchi.
Kwa mujibu wa tovuti ya ic-el sherehe hizo zimepangwa na jumuiya ya wanawake ya kituo hicho na zinatazamiwa kuanza saa 12 na nusu jioni.
Sherehe hizo ambazo zitawashirikisha wanawake tu zitajumuisha ratiba tofauti ambazo zimeandaliwa na wasimamizi wa kituo hicho cha Kiislamu kwa ajili ya kuadhimisha uzawa wa Bibi Fatima na Siku ya Wanawake. 791141
captcha