IQNA

Syria yalaani jinai za utawala wa Kizayuni Golan, Palestina na Lebanon

19:12 - May 17, 2011
Habari ID: 2123591
Wizara ya Mambo ya Nje ya Syria imelaani vikali jinai zinazotekelezwa na utawala haramu wa Israel katika milima yake inayokaliwa kwa mabavu na utawala huo ya Golan, na katika nchi za Palestina na Lebanon.
Kwa mujibu wa shirika la habari la Kuwait KUNA, Syria imeitaka jamii ya kimataifa kufanya juhudi za kusimamisha jinai za utawala huo katika maeneo yaliyotajwa.
Taarifa ya wizara hiyo imetolewa kufuatia shambulio lilolofanywa hivi karibuni na utawala huo wa Kizayuni dhidi ya watu waliokuwa wakiandamana hapo siku ya Junapili dhidi ya utawala huo huko kusini mwa Lebanon kwa mnasaba wa kukumbukwa mwaka wa 63 wa kubuniwa rasmi utawala huo ghasibu yaani Siku ya Nakama. 792860
captcha