IQNA

Pakistan kuandaa kongamano kubwa zaidi za Taasisi Ndogo za Fedha za Kiislamu

17:00 - May 21, 2011
Habari ID: 2125838
Taasisi ya Alhuda ya Benki za Kiislamu na Uchumi kwa kushirikiana na taasisi ya Ukhuwwat imeandaa Kongamano la Kimataifa la Taasisi Ndogo za Fedha za Kiislamu Juni 13 mjini Islamabad.
Kongamano hilo litajumuisha wajumbe 800 kutoka nchi 12.
Lengo la kongamano hilo limetajwa kuwa ni kubuni mpango wa kukabiliana na umasikini katika kiwango cha kitaifa na kimataifa.
Wajumbe kutoka nchi kama vile Malaysia, Yemen, Afghanistan, Indonesia na Mauritius watahudhuria kikao hicho. Mada zitakazojadiliwa kuhusu Taasisi Ndogo za Fedha za Kiislamu ni kama vile mbinu za kupunguza umasikini, Zakat, Waqfu, mbinu za kisasa katika uendesha Taasisi Ndogo za Fedha za Kiislamu, matumizi ya teknolojia ya kisasa na Taasisi Ndogo za Fedha za Kiislamu katika jamii zisizokuwa za Waislamu.
795314
captcha