IQNA

12:20 - May 26, 2011
Habari ID: 2128635

Kikao cha kuainisha nyakati za swala kufanyika Senegal

Kikao cha kuainisha nyakati za swala kwa mujibu wa sheria za Kiislamu kitafanyika tarehe 30 Mei katika mji mkuu wa Senegal, Dakar.

Kikao hicho kitasimamiwa na Kituo cha Utafiti na Mafunzo ya Kiislamu (CERFI) kikihudhuriwa na mamia ya maimamu wa swala za jamaa wa misikiti ya Dakar na miji ya kandokando yake.
Lengo la kuitishwa kikao hicho ni kutazama upya nyakati za swala za kila siku na kuainisha wakati mmoja wa kutolewa adhana kwa misikiti mbalimbali, kusimamisha swala za jamaa na kufanya mazungumzo kuhusu udharura wa kuwepo umoja kati ya wafuasi wa madhehebu mbalimbali za Kiislamu nchini Senegal.
Kikao cha utangulizi cha mpango huo kilifanyika wiki iliyopita na washiriki walikubaliana kukutana katika kikao cha wazi ambacho kitawashirikisha maimamu wote wa swala za jamaa kujadili maudhui hizo.
Ni vyema kukumbusha hapa kuwa baada ya Vita vya Pili vya Dunia na tawala za kikoloni nchini Senegal, makamanda wa kijeshi walibadilisha nyakati za swala katika misikiti mbalimbali, jambo ambalo limeendelea hadi hii leo katika miji mingi ya nchi hiyo na misikiti ya jiji la Dakar. 798130
captcha