IQNA

Waziri wa Fedha wa Jordan ataka kuimarishwa ushirikiano wa kiuchumi wa nchi za Kiislamu

12:19 - May 26, 2011
Habari ID: 2128711
Waziri wa Fedha wa Jordan Mohammad Abu Hammour ametoa wito wa kuimarishwa uhusiano wa kiuchumi wa nchi za Kiislamu ili kukabiliana na changamoto za kiuchumi.
Aliyasema hayo mjini Amman hivi karibuni katika hotuba aliyotoa kwa niaba ya Mfalme Abdullah wa nchi hiyo katika sherehe za ufunguzi wa Kongamano la Kimataifa la Uwekezaji katika Nchi za Kiislamu.
Alisisitiza kuwa nchi za Kiislamu zinapaswa kuwa na mikakati ya pamoja ya kutekeleza makubaliano yote ya Jumuiya ya Nchi za Kiislamu OIC kuhusu uimarishwaji uhusiano wa kibiashara na kichumi kati ya nchi wanachama.
Aidha Abu Hammour amesisitiza kuwa kuna udharura wa kuongeza uwekezaji na mabadilishano ya kibiashara kati ya wanachama wa OIC. Amesema nchi za Kiislamu zinapaswa kupasisha sheria za kuwavutia wawekezaji.
798267
captcha