IQNA

Mkutano wa benki na taasisi za kifedha za Kiislamu kufanyika Singapore

12:24 - May 26, 2011
Habari ID: 2128713
Karibu wataalamu 450 watakutana nchini Singapore kujadili muelekeo na fursa katika sekta ya kifedha ya Kiislamu barani Asia katika mkutano wa pili wa Kila mwaka wa kimataifa wa Mfumo wa Benki za Kiislamu kuanzia Juni 8-9 nchini Singapore.
Kuna benki na taasisi za kifedha za Kiislamu 430 katika zaidi ya nchi 75 duniani huku benki 191 za kawaida zikiwa na 'dirisha' la huduma za kibenki za Kiislamu.
Kuimarisha mfumo wa kifedha wa Kiislamu Mashariki ya Kati na Asia ni mambo ambayo yamechangia kuenea kimataifa benki za Kiislamu.
Mfumo wa kifedha wa Kiislamu umekuwa kwa kasi sana katika uga wa kimataifa na sasa umekita mizizi katika maeneo mbalimbali ya dunia.
Mkurugenzi wa Mkutano wa Kimataifa wa Mfumo wa Banki za Kiislamu David McLean amesema kikao cha Asia mwaka huu wa 2011 kitakachofanyika nchini Singapore kitajadili ushirikiano wa nchi zinazopakana ili kutoa msukumo katika ustawi wa kimataifa. 'Tunataka kuimarisha nafasi ya Asia kama kituo cha mfumo wa kifedha wa Kiislamu', amesema McLean.
797790


captcha