IQNA

Barua ya Mashia wa Bahrain ya kukarabatiwa misikiti iliyobomolewa

12:03 - May 28, 2011
Habari ID: 2129420
Idara ya Wakfu ya Mashia wa Bahrain imemwandikia barua Mfalme Hamad bin Isa Aal Khalifa wa nchi hiyo ikimtaka atoe amri ya kujengwa na kukarabatiwa mara moja misikiti iliyobomolewa hivi karibuni na askari jeshi wa nchi hiyo wakishirikiana na wa utawala wa Saudia.
Barua hiyo inazungumzia kuharibiwa kabisa misikiti 28 ambayo inataka ikarabatiwe mara moja na kurejeshwa kwenye hali iliyokuwepo kabla ya kubomolewa. Idara ya Wakfu ya Mashia wa Bahrain inasema kuwa baada ya misikiti hiyo kuharibiwa na askari hao kandamizi imebadilishwa na kuwa sehemu ya makumbusho. Idara hiyo inaendelea kusema kuwa misikiti mingine saba na huseiniyya nane na vilevile maeneo mawili ya makaburi ya Mashia yameharibiwa kutokana na hujuma ya kinyama ya askari hao na kwa hivyo yanapaswa kukarabatiwa mara moja.
Tunakumbusha hapa kwamba maandamano ya Waislamu wa Bahrain yangali yanaendelea dhidi ya utawala wa kifalme wa nchi hiyo, maandamano yanayoutaka ufutilie mbali hukumu ya kifo iliyotolewa dhidi ya baadhi ya waandamanaji. Waandamanaji vilevile wanataka askari vamizi wa Saudia waondoke mara moja katika ardhi ya Bahrain. 799094
captcha