Wizara hiyo imesema kuwa kituo hicho kitajengwa katika eneo la Suhban mjini humo. Kamati hiyo imesema ombi hilo limetekelezwa katika kalibu ya amri ya mfalme wa nchi hiyo ya kujengwa kituo cha Qur'ani Tukufu, shirika la chapa na tarjumi ya Qur'ani katika lugha tofauti pamoja na kituo cha utafiti wa Qur'ani mjini Kuwait.
Majengo mengine yanayotazamiwa kujengwa kwenye kituo hicho ni pamoja na kituo cha mabadilishano ya habari za Kiislamu na Qur'ani Tukufu, kituo cha mijadala ya wataalamu wa Kiislamu wa kitaifa, kieneo na kimataifa kuhusu Qur'ani, jumba la mikutano ya kielimu, jumba la maonyesho ya chapa za kale za Qur'ani na maktaba ya kitaalamu kuhusu masuala mbalimbali ya Qur'ani. 800808