Vikosi vya utawala wa Kizayuni wa Israel viliwaua shahidi raia 28 na kuwajeruhi wengine 350 hivi karibuni wakati wa kumbukumbu ya mwaka wa 44 tokea Wazayuni wateke ardhi zaidi za Waarabu. Siku hiyo hujulikana kama Siku ya Naksa au Siku ya kushindwa.
Utawala Wa Kizayuni umekuwa ukitelekeza jinai na mauaji ya umati dhidi ya Wapalestina kwa miaka 63. Katika kipindi hicho Wazayuni wamewapkonya Wapalestina haki zao ikiwa ni pamoja na kupora ardhi zao, imesema taarifa ya Umoja wa Nchi za Kiarabu.
Utawala wa Kizayuni umekaidi amri ya Umoja wa Mataifa ya kuondoka katika ardhi za Wapalestina unaozikalia kwa mabavu.
805129