IQNA

Gavana wa Quds alaani ujenzi wa jumba la makumbusho la Wazayuni juu ya makaburi ya Waislamu

14:18 - June 11, 2011
Habari ID: 2136022
Adnan al-Husseini, gavana wa Kipalestina wa mji mtakatifu wa Quds amelaani vikali uamuzi wa watawala wa Israel wa kujenga jumba la makumbusho juu ya makaburi ya Waislamu ya Ma'man magharibi mwa mji huo.
Al-Husseini amelaani kuharibiwa kwa maeneo ya Kiislamu katika eneo lilotajwa kwa ajili ya kujengwa jumba la makumbusho la Wazayuni na kuongeza kuwa hiyo ni ishara ya wazi ya kuendelea kuyahudishwa mji huo mtakatifu. Amesema watawala wa Israel wamekuwa wakibainisha taratibu uamuzi wao wa kujenga jumba hilo la makumbusho na kwamba wameazimia kubomoa kabisa makaburi hayo ya kihistoria kwa ajili ya kuandaa uwanja wa kujengwa jumba hilo.
Al- Husseini amesema awali ardhi ya makaburi hayo ilikuwa na ukubwa wa hekari 205 na kwamba hivi sasa imeporwa na Wazayuni na imebakia hekari 15 tu. Ameongeza kuwa Wazayuni wamekuwa wakipora na kuharibu maeneo ya ibada ya Waislamu ili kufuta kabisa utambulisho wa Kiislamu na Kiarabu wa maeneo hayo. 805950
captcha