Kwa mujibu wa tovuti ya marocjournal, shakhsia wa kisiasa na kiutamaduni pamoja na vyama tofauti vya nchi hiyo vimeridhishwa na hatua ya kuashiriwa wazi jambo hilo katika rasimu ya katiba mpya ya nchi hiyo.
Kikizungumzia suala hilo, Chama cha Umoja na Marekebisho cha Morocco kimepongeza hatua hiyo iliyochukuliwa na mfalme wa nchi hiyo na kuongeza kuwa itaimarisha umoja wa kitaifa nchini na kufanya mafundisho ya Kiislamu kuwa nguzo muhimu ya uendeshaji wa serikali. Chama hicho kimesema, watu wa dini tofauti wamekuwa wakiishi pamoja kwa amani na utulivu na kusisitiza kuwa katiba mpya ya nchi hiyo inapasa kusimama kwenye misingi yake mikongwe ya historia ya Kiislamu na Kiarabu. Kimesema, kutangazwa Uislamu kuwa dini rasmi ya nchi hiyo kutachangia pakubwa katika kulinda utambulisho wa historia hiyo.
Wasomi na wanazuoni wa Morocco pia wamekuwa wakitoa taarifa tofauti na kuunga mkono hatua ya kutangazwa Uislamu kuwa dini rasmi ya nchi hiyo.
Kufuatia maandamano ambayo yamekuwa yakifanywa na wananchi wa nchi za Karabu dhidi ya tawala zao za kidikteta na zinazoegemea upande wa madola ya Magharibi, wananchi wa Morocco pia wamekuwa wakifanya maandamano ya kutaka katiba yao ifanyiwe marekebisho kwa lengo la kupewa sauti na uhuru zaidi wa kidini na kiraia, jambo ambalo limempelekea mfalme wa nchi hiyo kubuni kamati ya kutazama upya katiba hiyo. 808014