IQNA

Tamasha kubwa ya filamu ya Uislamu na Imam Hussain (as) kufanyika Karbala

19:26 - June 20, 2011
Habari ID: 2141475
Mtayarishaji mashuhuri wa filamu wa Iraq Jamal Amin al Hassani amesema kuwa anatayarisha mpango wa kufanya tamasha ya kimataifa ya filamu ya Uislamu na Imam Huusein (as) katika mji mtakatifu wa Karbala.
Jamal Amin al Hassani amesema tamasha hiyo itahusu filamu itakayozungumzia Uislamu kwa ujumla na Imam Hussein (as).
Amesema kwa sasa Iraq ina uwezo wa kutengeza filamu kuhusu Bwana wa Vijana wa Peponi Imam Hussein bin Ali (as).
Amin al Hassani ambaye amerejea nchini Iraq baada ya kuishi nje ya nchi kwa kipindi cha miaka 20 amesema alikuwa na shauku kubwa ya kurejea nchini hususan baada ya kuondolewa madarakani utawala wa Saddam Hussein. Amesema kuwa amefurahishwa kuona harakati za kidini na za vyombo vya habari kama televisheni ya Karbala na redio ya al Raudhatul Hussainiyyah ambavyo amesema vinawafaidisha watu na kuwaelimisha mengi kuhusu Imam Hussein, harakati ya Ashura na madhehebu ya Kiislamu ya Shia. 811972


captcha