Is’haq Abdollahi, aliyewakilisha Iran katika kipengele cha tilawa ya Qur’an, alishinda nafasi ya pili kwa heshima kubwa.
Aidha, Mehdi Barandeh, mhifadhi wa Qur’an kutoka Iran, alishika nafasi ya nne katika kipengele cha hifdh ya Qur’an nzima.
Mashindano haya yalifanyika kuanzia tarehe 18 hadi 20 Disemba mjini Dhaka, mji mkuu wa nchi hiyo ya Asia Kusini, yakihusisha maqari na mahafidh kutoka nchi 30.
Miongoni mwa nchi zilizoshiriki ni pamoja na Iran, Saudi Arabia, Bangladesh, India, Misri, Indonesia, Malaysia, Pakistan, Algeria, Brunei, Kuwait na Tanzania.
Barandeh tayari amewahi kushinda nafasi ya kwanza katika mashindano ya 45 ya kimataifa ya Qur’an nchini Saudi Arabia. Vilevile, Abdollahi ana historia ya mafanikio, ikiwemo kushika nafasi ya kwanza katika mashindano ya 23 ya kimataifa ya Qur’an nchini Urusi.
Baada ya kushiriki katika halaqa mbalimbali za Qur’an wiki hii nchini Bangladesh, wawili hao wanatarajiwa kurejea Iran Jumamosi, kwa baraka za Mwenyezi Mungu.
4324062