Mawaziri hao wanatazamiwa pia kuchukua uamuzi kuhusu kikao cha 57 cha viongozi wa Jumuiya ya Nchi za Kiislamu. Mkutano huo uliokuwa umepangwa kufanyika Misri uliakhirishwa kwa sababu ya mwamko wa Kiislamu mwezi Januari nchini humo.
Masuala ya Libya, Pakistan na Somalia yanatazamiwa kutawala ajenda ya OIC na vilevile suala la Afghanistan linatazamiwa kupewa umuhimu. Ajenda nyingine ya kikao hicho ni kubuniwa Tume ya Haki za Binaadamu ya OIC.
Nchi za OIC zinazokumbwa na misukosuko ni pamoja na Yemen, Bahrain, Jordan, Libya na nchini Misri bado hali si shwari.
Kazakhstan ilichukua uenyekiti wa OIC mwaka 2011. Jumuiya ya Nchi za Kiislamu ina wanachama 57.
812523