IQNA

Malaysia, mwenyeji wa mkutano wa kimataifa wa “Uislamu Barani Afrika”

11:49 - June 30, 2011
Habari ID: 2146843
Mkutano wa Kimataifa wa Uislamu Barani Afrika utafanyika tarehe 19 hadi 21 Julai katika Chuo Kikuu cha Kiislamu cha Kimataifa cha Malaysia mjini Kuala Lumpur.
Mkutano huo utasimamiwa na Chuo Kikuu cha Kiislamu cha Kimataifa cha Malaysia (IIMU), Taasisi ya Kimataifa ya Ustaarabu na Fikra za Kiislamu (ISTAC), Muungano wa Vyuo Vikuu vya Ulimwengu wa Kiislamu (FUIW) na Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Jumuiya Ushirikiano wa Kiislamu ISESCO.
Lengo la mkutano huo limetajwa kuwa ni kuchunguza historia na utamaduni wa Uislamu barani Afrika, kupanua zaidi mazungumzo na mahusiano kati ya Uislamu ma dini nyingine za Afrika, kuanzisha kanali ya mawasiliano kati ya watafiti na wanafikra kuhusu Uislamu barani Afrika na kadhalika.
Masuala mengine yatakayojadiliwa katika mkutano huo ni pamoja na maendeleo na changamoto za utafiti na kupata elimu ya Kiislamu barani Afrika, kukua na kuenea Uislamu barani Afrika, turathi za Kiislamu huko Afrika, vyanzo vya Kiislamu barani Afrika, taasisi za kisiasa na vituo vya elimu za Kiislamu Afrika, mipango ya masomo ya Kiislamu katika vyuo vikuu na shule, uchunguzi juu ya utekelezaji wa Uislamu barani Asia na Afrika na uhusiano kati ya Uislamu na dini nyingine katika jamii za Kiafrika. 817662
captcha