Shirika la habari la Ufaransa limeripoti kuwa baada ya kupasishwa rasimu hiyo sasa katiba mpya ya Tunisia itakuwa na kipengee kinachopiga marufuku kuanzishwa uhusiano wa kawaida na utawala wa Kizayuni wa Israel.
Mwenyekiti wa Kamati ya Marekebisho ya Kisiasa ya Tunisia Iyadh bin Ashur ameitaja hatua ya kupigwa marufuku uhusiano wa kisiasa na kibiashara na utawala wa Kizayuni wa Israel na ulazima wa kuwaunga mkono wananchi wanaodhulumiwa wa Palestina kuwa ni habari ya kufurahisha.
Suala la kuanshwa uhusiano wa kawaida kati ya Tunisia na utawala ghasibu wa Israel lilikuwa limezusha makelele na mvutano mkubwa katika Kamati Kuu ya Kutekeleza Malengo ya Mapinduzi ya Tunisia. 818322