IQNA

Rais Ahmadinejad: Kuimarishwa uhusiano wa Iran na Imarati kutavunja njama za maadui

15:57 - July 10, 2011
Habari ID: 2151763
Rais Mahmoud Ahmadinejad wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema uhusiano wa Iran na Umoja wa Falme za Kiarabu ni wa kidugu.
Amesema nchi hizi mbili hazipaswi kuyaruhusu madola ya kibeberu kupanga njama katika eneo la Ghuba ya Uajemi.
Rais Ahmadinejad ameyasema hayo mjini Tehran baada ya kupokea vitambulisho vya balozi mpya wa Imarati nchini. Katika kikao hicho Rais Ahmadinejad amesisitiza umuhimu wa kustawisha uhusiano kati ya Tehran na Abu Dhabi. Amesema uhusiano wa nchi hizi mbili unaweza kuwa mfano wa kuigwa na nchi za eneo hilo na hivyo kuvunja njama za maadui. Amesema kuwa Marekani na waitifaki wake ni maadui wa nchi za eneo hilo.
Kwa upande wake balozi mpya wa Umoja wa Falme za Kiarabu nchini Iran Seif Mohammad bin Obeid amesema nchi yake inataka kustawisha uhusiano na Iran katika nyanja zote.
822774
captcha