IQNA

Maonyesho ya nakala ya kale ya Qur'ani mjini Riyadh

17:26 - July 11, 2011
Habari ID: 2152754
Nakala nadra sana ya Qur'ani iliyoandikwa katika zama za utawala wa Kiothmani itaonyeshwa katika Jumba la Makumbusho la Riyadh, Saudi Arabia.
Kituo cha Alyaum kimeripoti kuwa Jumba la Makumbusho la Hermitage la Russia linakusudia kufanya maonyesho katika Jumba la Makumbusho la Kitaifa la Riyadh na kuonyesha nakala hiyo nadra ya Qur'ani kwa watazamaji.
Maonyesho hayo yatajumuisha athari na vitu vya kale na vya kihistoria vilivyokusanywa katika Mashariki ya Karibu.
Mkurugenzi wa Jumba la Makumbusho la Hermitage amesema mipango inafanyika kwa ajili ya kuonyesha nakala ya Qur'ani iliyoandikwa kenye kipindi cha utawala wa Kiothmani katika Jumba la Makumbusho la Riyadh, Saudi Arabia.
Eneo la Mashariki ya Karibu linajumuisha nchi za Magharibi mwa Asia kama nchi za Kiislamu za Urusi ya zamani, Palestina, Jordan, Syria, Lebanon, Uturuki, Cyprus na Iraq. 823519

captcha