IQNA

Mahakama ya Ulaya yaunga mkono marufuku ya ujenzi wa minara ya misikiti

23:55 - July 11, 2011
Habari ID: 2152770
Mahakama ya Ulaya ya Haki za Binadamu imetoa hukumu ya kupinga rufaa ya Waislamu wa Uswisi kuhusu uamuzi wa nchi hiyo wa kupiga marufuku ujenzi wa minara ya misikiti.
Katika hukumu hiyo ya siku ya Ijumaa ambayo imesubiriwa kwa mudara mrefu, sababu iliyotolewa ni kuwa kesi hiyo haijafikishwa katika mahakama za Uswisi.
Mmoja kati ya waliowasilisha kesi hiyo Hafid Ouardiri aliyekuwa wakati moja msemaji wa Msikiti wa Geneva amesema alishuku mahakama ingetoa hukumu kama hiyo. Amesema kesi hiyo sasa itawasilishwa katika mahakama ya Uswisi.
Inafaa kuashiria hapa kuwa, tarehe 29 Novemba mwaka 2009, iliitishwa kura ya maoni nchini Usiwisi, ambapo asilimia 57 ya wananchi wa nchi hiyo waliunga mkono upigaji marufuku wa ujenzi wa minara ya misikiti nchini humo, hatua ambayo imepingwa vikali na Waislamu katika pembe mbalimbali duniani.
Kura hiyo ya maoni ya kupiga marufuku ujenzi wa minara ya misikiti ilihesabiwa kama moja ya njama za walio na chuki dhidi ya Uislamu barani Ulaya.
823596
captcha