IQNA

Waislamu Marekani kufunzwa kuhusu mfumo wa kifedha wa Kiislamu

17:00 - July 18, 2011
Habari ID: 2155958
Ni hatua gani ichukuliwe kuwafunza Waislamu milioni 7 Marekani kuhusu mfumo wa kifedha wa Kiislamu? Pengine kuwafunza viongozi 100 mashuhuri wa kidini ni hatua ya awali.
Haya ndio mafanikio ya waanzilishi wa mradi wa Mfumo wa Kifedha wa Kiislamu Marekani (American Islamic Finance-AIF).
Mfumo wa Kifedha wa Kiislamu Marekani ni mradi wa pamoja wa Taasisi ya Mfumo wa Kifedha wa Kiislamu ya Ethica, Guidance Financial na Jumuiya ya Kiislamu ya Amerika Kaskazini. Mradi huo unalenga kustawisha mfumo wa kifedha wa Kiislamu miongoni mwa jamii za Kiislamu Marekani na Canada.
Mradi huo unajumuisha mafunzo ya miezi miwili kwa Maimamu na inatarajiwa kuwa kozi hiyo itakuwa ikifanyika kila mwaka.
827284
captcha