Kituo cha habari cha Nun kimeripoti kuwa jumuiya za kimataifa zinazofuatilia hali ya Bahrain zina habari kuhusu hatua ya Waziri Mkuu wa nchi hiyo Khalifa bin Salman na Waziri wa Mambo ya Ndani Rashid ambaye ni mkwe wake ya kuunda genge le kigaidi kwa ajili ya kufanya mauaji dhidi ya viongozi wa Waislamu wa madhehebu ya Shia wanaopinga utawala wa kifalme wa Aal Khalifa.
Vilevile kituo cha habari cha Mir'atul Bahrain kimeripoti kuwa mfalme wa Bahrain pia anajua habari hiyo.
Duru za kuaminika zinasema kuwa baada ya Mwenyekiti wa Kamati ya Kimataifa ya Kuchunguza Ukweli kuhusu Bahrain kupata habari ya kuundwa kundi hilo la kigaidi, askari usalama wa nchi hiyo wameamua kusimamisha kwa muda mpango.
Habari zinasema kuwa utawala wa Bahrain umesambaza silaha nyingi za kisasa kati ya wahajiri wa kiasia na baadhi ya Waarabu waliohamia nchini humo kwa nia ya kupewa uraia. 829805