Jumuiya hiyo imepanga kugawa viroba 5000 vya chakula cha futari kwa Waislamu wanaofunga wa Palestina katika mwezi wa Ramadhani na kwa msingi huo imewataka raia wa Ufaransa kutoa misaada yao ya kifedha kwa ajili ya kufanikisha mpango huo.
Mwaka jana Jumuiya ya Muslim Hands iligawa viroba 1200 vya chakula cha futari katika msikiti wa al Aqsa na zaidi ya viroba 600 vya chakula katika misikiti ya Ramallah, Bait Laham, al Khalil na Nablos.
Taarifa ya Muslim Hands imesema Euro 60 za kila raia wa Ufaransa zinaweza kudhamini chakula cha Wapalestina 8 katika mwezi mtukufu wa Ramadhani. 829579