Watumiaji Waarabu wa mtandao wa kijamii wa Facebook wameanzisha kurasa nyingi katika mtandao huo wakiwataka watu kususia filamu hiyo kutokana na kuwavunjia heshima wajukuu hao wa Mtume (saw) kwa kuonyesha sura za watukufu hao na kupotosha historia ya Kiislamu.
Filamu ya al Asbat haijaanza kuonyeshwa katika kanali za televisheni za satalaiti lakini televisheni kadhaa za Misri zinapanga kuionyesha katika mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Jumuiya kadhaa za Kiislamu ikiwa ni pamoja na Taasisi ya Utafiti wa Kiislamu ya al Azhar ya Misri na maulamaa wa Kiislamu kutoka pembe mbalimbali duniani wamezitaka kanali za televisheni kutoonyesha filamu hiyo na kutangaza kuwa watafungua mashtaka dhidi ya televisheni itakayoirusha hewani.
Mbali na al Azhar, Jumuiya ya Kimataifa ya Fiqhi ya Kiislamu na maulamaa wa madhehebu ya Shia pia wametoa fatuwa wakiharamisha kuonyeshwa sura za Mitume wa Mwenyezi Mungu, masahaba wa Mtume (saw) na Ahlulbait (as) katika filamu na michezo ya televisheni. Filamu hiyo inawatetea Muawiyah bin Abi Sufiyan na mwanawe Yazid ambao waliwaua wajukuu wa Mtume Muhammad (saw) Imam Hassan na Hussein (as). 830748