Taarifa ya baraza hilo imelaani mashambulizi ya kigaidi yaliyotokea nchini Norway na kusema kuwa matukio yaliyojiri mjini Oslo yanapaswa kuwa somo kwa watu wote na kwamba imebainika kuwa makundi yanayofanya jinai hizo za kutisha hayasiti kufanya lolote kwa ajili ya kukamilisha malengo yao ambayo ni kukabiliana na Uislamu na tamaduni tofauti barani Ulaya.
Baraza la Waislamu wa Britani limetuma salamu za rambirambi kwa familia za wahanga wa mauaji ya kigaidi ya Norway na kusisitiza kuwa kwa mujibu wa aya za Qur'ani Tukufu kumuua mtu mmoja asiyekuwa na hatia ni sawa na kuua wanadamu wote na kwamba vitendo kama hivyo vya kigaidi vinalaaniwa vikali ya dini ya Kiislamu.
Sehemu nyingine ya taarifa hiyo imesema: Mashambulizi ya kigaidi ya Norway yanapaswa kuzusha swali kwamba wale wanaoendesha hujuma za propaganda chafu za kuwatisha watu na Uislamu na kueneza fikra hizo barani Ulaya wamekuwa na mchango gani katika matukio hayo ya kigaidi? 831836