Katika mahojiano na mwandishi wa IQNA, Sheikh Muhdhar amesema kamati maalumu ya kuutafuta mwezi itakutana katika mji wa Mombasa tarehe 31 ambapo itapokea ripoti kutoka eneo lote la Afrika Mashariki.
Amesema iwapo Mwezi utaonekana Julai 31 basi siku ya pili yake itatangazwa kuwa tarehe ya kwanza ya Ramadhani la sivyo siku hiyo itatangazwa kuwa tarehe 30 Shaaban. Kadhi Mkuu wa Kenya amesema kwa miaka mingi Waislamu wa Afrika Mashariki wamekuwa wakitegemea mwezi mwandamo wa eneo hilo kuanza au kumalizika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani na hivyo amesema sera hiyo itaendelea.
Wakati huo huo Kadhi Mkuu wa Kenya amesema kuwa Waislamu wenye uwezo nchini Kenya wanakusanya misaada kuwasaidia wenzao wanaokumbwa na baa la njaa nchini humo na nchi jirani ya Somalia.
832886