IQNA

10:58 - July 31, 2011
Habari ID: 2162448

OIC yataka kuweo mapambano dhidi ya makundi yenye misimamo mikali Ulaya

Katibu Mkuu wa Jumuisya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) Ekmeleddin Ihsanoglu amezitaka jumuiya za kimataifa kupambana na makundi yenye misimamo mikali barani Ulaya.

Ihsanoglu amesema jumuiya za kimataifa zinapaswa kutazama upya shughuli zao baada ya mashambulizi ya kigaidi ya Norway na kusisitiza kuwa mashambulizi hayo ya kigaidi yamefanywa na mtu ambaye ana misimamo ya chuki na kinyongo dhidi ya kuwepo tamaduni mbalimbali barani Ulaya hususan Uislamu.
Katibu Mkuu wa OIC amesema mashambulizi ya kigaidi ya Norway yamebainisha chuki na uhasama wa makundi ya watu wenye misimamo ya kufurutu mipaka dhidi ya Uislamu na Waislamu na kwamba uhasama huo ni kama sumu inayoua ambayo inatishia raia wengine wa Ulaya kama inavyowalenga Waislamu.
Prf. Ihsanoglu amezitaka jumuiya za kimataifa kuchukua hatua za kukabiliana vikali na mukundi yenye misimamo ya kufurutu ada kote duniani. 834218



captcha