Katika ujumbe wake, Rais Ahmadinejad ameelezea matumaini kuwa katika mwezi huu mtukufu, udugu na umoja utaimarishwa katika umma wa Kiislamu kwa mujibu wa mafundisho ya Qur'ani Tukufu na Suna ya Mtume SAW.
Aidha ameelezea matumaini kuwa mwezi huu mtukufu utakuwa fursa ya kuwatetea waliodhulumiwa ili hatimaye uadilifu na amani ya kudumu ienee duniani.
Rais Ahmadinejad amewatakia afya njema na fanaka viongozi wa nchi za Kiislamu na Waislamu kote duniani.
834933