Utafiti huo umechunguza faida za kimwili na kijamii za Saumu pamoja na njia sahihi za kutekeleza nguzo hii ya dini.
Utafiti huo unasema Saumu kwanza huakisiwa katika mtu binafsi pale anapojiepusha na dhambi za matamshi kama vile kudanganya, kusengenya na kutoa tuhuma kwani asipofanya hivyo Saumu itakuwa haina maana mbele ya Mwenyezi Mungu.
Kujiepusha na dhambi katika mwezi huu mtukufu hatimaye humsaidia mtu binafsi kujitakasa kutokana na madhambi hayo. Nukta nyingine iliyotajwa ni kupungua jinai katika Mmwezi mtukufu wa Ramadhani. Utafiti huo pia unaashiria uhusiano kati ya Saumu na utulivu na kuongezeka takwa.
Utafiti huo uliofanywa kwa mujibu wa mafundisho ya Ahul Bayt AS pia umegundia kuwa kuna faida nyingi za saumu katika jamii kama vile kupunguza umasikini, jinai, kuimarisha uchumu na kuzidisha moyo wa huruma.
838032