Jumuiya hiyo imetangaza kuwa itashirikiana na wanamapinduzi wengine wa nchi hiyo katika kuandaa tamasha muhimu siku ya Ijumaa ambalo litapewa jina la 'Hakuna Kurudi Nyuma.' Jumuiya hiyo imeutaka utawala wa Bahrain uwaachilie huru mara moja wafungwa wote wa kisiasa waliotiwa mbaroni katika harakati za hivi karibuni za kupigania demokrasia na uhuru wa kujieleza nchini humo.
Vilevile imelaani hatua ya mashirika na idara za serikali na zisizo za serikali za kuwafukuza kazini wafanyakazi wanaoshukiwa kuwa wapinzani wa watawala hao na kutaka wafanyakazi hao warejeshwe makazini kwao mara moja bila kubaguliwa kwa misingi ya madhehebu.
Katika siku za hivi karibuni wananchi wa Bahrain wamekuwa wakifanya maandamano dhidi ya ukandamizaji unaofanywa dhidi yao na mfumo wa ufalme wa ukoo wa Aal Khalifa na uingiliaji wa kijeshi wa utawala wa Saudi Arabia katika masuala ya ndani ya nchi hiyo ndogo ya Kiarabu. 840869