Hayo yalisema hapo jana Ijumaa na Abu Sharif, mwakilishi wa Harakati ya Jihad al-Islami ya Palestina katika maonyesho ya Qur'ani Tukufu yanayoendelea hapa mjini Tehran. Amesema Waislamu wa Iran, Uturuki na nchi za Kiarabu ndio msukumo mkubwa unaoathiri kwa kiwango kikubwa ulimwengu wa Kiislamu. Ameongeza kuwa Iran, kwa Uongozi wa Imam Khomeini (MA), ilianza kuchangia sehemu kubwa ya usuluhishaji na utatuzi wa masuala ya ulimwengu wa Kiislamu miaka 32 iliyopita baada kuangushwa mfumo wa kitaghuti wa Shah nchini.
Abu Sharif ameendelea kusema kuwa wananchi wa Uturuki hata baada ya kubuniwa mfumo wa usekula nchini humo wamekuwa katika mstari wa mbele wa kupigania masuala ya Palestina inayokaliwa kwa mabavu na utawala haramu wa Israel.
Ameongeza kuwa wananchi Waislamu katika nchi za Kiarabu wamekuwa wakipigania masuala ya Kiislamu katika nchi zao lakini kwamba watawala dhalimu wa nchi hizo hawajakuwa wakiwapa nafasi nzuri ya kufikia malengo yao.
Abu Sharif ameelezea matumaini yake kwamba kwa kuendelea kuanguka tawala hizo katika nchi za Kiarabu, Palestina itaanza kudhihiri na kuzingatiwa zaidi katika mkondo wa matukio ya Kiislamu. Amemaliza kwa kusema kuwa sababu kuu ya hali ya kusikitisha ya hivi sasa ya Waislamu duniani sio nguvu ya nchi za Magharibi wala uadui dhidi ya Uislamu, bali ni udhaifu mkubwa wa umma wa Kiislamu katika karne kadhaa zilizopita, hali ambayo kwa bahati nzuri amesema imeanza kubadilika taratibu. 841829