Sherehe hizo zilizotangazwa kuanza rasmi na Hamid Ali Shah Musawi, Kiongozi wa Mashia wa Pakistan, zilifanyika sambamba na kuadhimishwa Siku ya Kimataifa ya Amani katika nchi hiyo.
Mashia wa Pakistan wamemuenzi na kumsifu Imam Hassan Mujtaba (as) katika sherehe hizo zilizofanyika kwa namna mbalimbali kupitia mikutano, seminari, karamu, maonyesho na mikusanyiko. Wasomi, wanafikra na wanazuoni wa Kiislamu walitoa hotuba mbalimbali kusifu na kuzungumzia maisha ya mtukufu huyo wa Nyumba ya Mtume (saw). Hamid Ali Shah Musa alitoa hutuba yake katika mji wa Rawalpindi. 845315