Hayo yalisemwa jana usiku na Sayyid Hashim Qassim Zadeh, mtaalamu wa masuala ya kiutamaduni na Qur'ani Tukufu katika Chuo Kikuu cha Tarbiyat Muallim cha Shahidi Mufattih mjini Rei. Sayyid Qassim Zadeh aliyasema hayo alipokuwa akijibu maswali kuhusiana na fikra za Mawahabi kuhusiana na suala hilo katika kikao maalumu cha maswali na majibu katika maonyesho ya 19 ya kimataifa ya Qur'ani Tukufu mjini Tehran.
Amesema Mawahabi wanaharamisha kutawasali na Mtume (saw) pamoja na Maimamu wa Ahlul Beit (as) pamoja na kuzuru makaburi yao katika hali ambayo aya ya 64 ya Surat an-Nisaa na ya 80 ya Sura at-Tauba zinazungumzia wazi umuhimu wa kutawasali na Maimamu pamoja na Mtume Mtukufu (saw).
Amesema uwahabi ni kundi la upotofu lililopachikwa katika ulimwengu wa Kiislamu na utawala wa Kizayuni pamoja na Uingereza, kundi ambalo amesema limezusha mambo yasiyokubalika kwenye dini, Qur'ani na Suna za Mtume (saw).
Sayyid Hashim Qassim Zadeh amesema kundi hilo limepotoka kidini na ndio maana likawa linatoa fatuwa za kushangaza zikiwemo zile zinazosema kuwa iwapo Muwahabi atawaua Mashia 7 ataingia peponi, likaharamisha mwanamke wa Kiislamu kufanya kazi ya mauzo na kudai kuwa iwapo Mwislamu atakufa kutokana na maradhi ya Ukimwi, tauni na kichaa cha nguruwe atakuwa shahidi. 847021